Nahodha na Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya England Harry Kane leo Jumatano (Novemba 23) atafanyiwa vipimo, ili kufahamu ukubwa wa jeraha linalomkabili.

Mshambuliaji huyo wa Klabu ya Tottenham alipatwa na majeraha ya Kifundo cha Mguu wake wa Kulia, akiwa katika Mchezo wa Kwanza wa Kundi B wa Fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Iran, juzi Jumatatu (Novemba 21).

Kane, mwenye umri wa miaka 29, alilazimika kutolewa katika Mchezo huo na nafasi yake kuchukuliwa na Callum Wilson, lakini baadae ilithibitika ana maumivu makali ya Kifundo cha Mguu.

Taarifa kutoka katika Kambi ya Timu ya Taifa ya England zinaeleza kuwa, Mshambuliaji huyo hana uhakika wa kucheza katika Mchezo wa Pili wa Kundi B dhidi ya Marekani, utakaounguruma Kesho Kutwa Ijumaa, na kinachosubiriwa ni majibu ya vipimo vya leo, ili kupata uhakika kama ataweza kutumiwa na Kocha Gareth Southgate.

Kane ameshaitumikia England katika mchezo 76 na kufunga mabao 51.

Wakati huo huo Kiungo James Maddison anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha England katika Mchezo dhidi ya Marekani, baada ya kukosa Mchezo wa Kwanza dhidi ya Iran, uliomalizika kwa The Three Lion kuibuka na ushindi wa 6-2.

OHCHR yaikatalia Serikali hukumu ya kifo
Waliofariki tetemeko la ardhi wafikia 268