Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka amemvaa mwanaharakati Mange Kimambi na kusema kuwa dada huyo anamchafua na kumgombanisha na viongozi wa nchi kwa kusambaza sauti ambayo si yake ambapo baadhi ya maneno kwenye hiyo sauti yamesikika yakisema Bunge sasa limeshikwa na kushindwa kufanya kazi yake.
Ole Sendeka amesema kuwa sauti iliyosambaa katika mitandao ya kijamii ikidaiwa kulidhalilisha bunge si yake bali ni michezo michafu iliyotengenezwa na upinzani kwa lengo la kumchafua na kumchonganisha na Serikali yake.
-
Kanisa tajiri Botswana lafungiwa
-
Lowassa uso kwa uso na Mbowe, amueleza kilichojiri Ikulu
-
Kibatala ajiengua uwakili kesi ya Wema Sepetu
“Akutukanaye hakuchagulii tusi, kupitia mitandao ya kijamii wameendelea kutengeneza na kusambaza ‘clip’ za kutafuta namna ya kunifarakanisha mimi na viongozi wa Serikali nataka niwaambieni ambazo mmeziona kwenye mitandao zinasambazwa na watu wa upinzani pamoja na sijui Mange Kimambi sijui kitu gani kile, ninaomba mzipuuze kwa kiwango kinachostahili maana zote ni uzushi mtupu” alisisitiza Ole Sendeka.
Ole Sendeka ameongea hayo kwenye Mkutano wa hadhara wa CCM katika kampeni za kumnadi mgombea wa Ubunge wa jimbo la Longido Arusha kwa chama hicho.
Kufuatia na sauti hiyo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kuiagiza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kujadili na kuchunguza kauli ya Mhe. Christopher Ole Sendeka inayodaiwa kudhalilisha Bunge.