Aliyekuwa wakili  wa kujitegemea, Peter Kibatala wa msanii maarufu wa filamu nchini Wema Sepetu, anayekabiliwa na kesi ya kukutwa na madawa ya kulevya aina ya bangi ameamua kujitoa kuitetea kesi hiyo.

Kibatala amewasilisha barua yake kwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ikitoa maelezo juu ya kujitoa katika kesi hiyo na amesema hawezi kuanika sababu zilizomfanya kuachana na kesi hiyo kwani ni kinyume na maadili ya kazi yake.

Hata hivyo mahakama hiyo imepokea barua ya utambulisho kutoka kwa wakili Albert Msando akiomba kuanza kumtetea Wema dhidi ya tuhuma ya dawa ya kulevya inayo mkabili.

”Mheshimiwa hakimu ninaomba muda wa kupitia jalada na mwenendo uliopita wa kesi hii, ili niweze kuanza kazi ya kumtetea mteja wangu” amesema Msando.

Aidha Kibatala amechukua nafasi hiyo kuiomba radhi mahakama ya hakimu mkazi kisutu kwa makwaruzano yaliyotokea pindi akiendesha kesi hiyo kwani anaamini ni katika kutimiza wajibu wake wa kikazi.

 

Lowassa uso kwa uso na Mbowe, amueleza kilichojiri Ikulu
JPM ateua mabalozi wapya