Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) limemuomba mambo mawili Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambayo ni kuwa na tume huru ya kweli na maridhiano pamoja na kurejesha mchakato wa kupata Katiba mpya.

Hayo yameombwa na Mwenyekiti wa baraza hilo John Pambalu wakati akizungumza na waandishi wa habari.

“Tunaishauri Serikali umuhimu wa kuwa na tume huru ya kweli na ya maridhiano, tume ambayo itataka kujiridhisha na kuchunguza kwa kina juu ya uovu wote ambao umefanyika,” amesema Pambalu.

Pia baraza hilo limemuomba  Rais Samia kuwaachilia huru wafungwa waliofungwa kwa ajili ya kesi za kisiasa kwa madai kuwa njia hiyo ni nzuri katika jamii.

Breaking: Ajali ya basi yaua 6 Manyara
Askofu Gwajima: Mama Samia ni Konki Fire