Bondia kutoka nchini Philippines, Manny Pacquiao atatundika gloves mwaka 2016 baada ya kuutumikia mchezo wa masumbwi tangu mwaka 1995.

Taarifa za kustaafu kwa bondia huyo zimetolewa na promota wake Bob Arum alipokua akihojiwa na muandishi wa habari wa tovuti ya TMZ huko West Hollywood nchini Marekani, siku ya jumanne.

Arum alisema Pacquiao amepanga kuchukua uamuzi huyo kwa kutaka kupumzika na kuwapisha wengine ili watambulike na kutimiza malengo yao kwenye mchezo wa masumbwi ambao umebeba vijana wengi duniani kote.

Promota huyo alisema bondia huyo anayetambulika kimataifa ana umri wa miaka 36 na mwezi Disemba mwaka huu atafikisha umri wa miaka 37, hivyo anaamini ni wakati mzuri kwake kufanya maamuzi ya kujiweka pembeni.

Wakati Pacquiao akiweka wazi mpango huo wa kutaka kujiweka pembeni kupitia kwa Promota wake, bado mashabiki wa masumbwi duniani wanaendelea kukumbuka namna walivyopambana na Floyd Mayweather, May 2 na kushindwa kwa point huko nchini Marekani.

Hata hivyo Pacquiao bado anaendelea kubebwa na rekodi yake ya kupambana ulingoni mara 65 na kushinda mara 57, kupoteza mara 6 na kupata matokeo ya sare mara 2.

Katika mapambano aliyoshinda, Pacquiao aliwahi kuwagaragaza wapiznani wake kwa KO mara 38.

De Gea Akamilisha Usajili UEFA
Joh Makini Atoa Mtazamo Wake Katika Siasa Zinazoendelea