Joh Makini ameelezea msimamo wake katika mkondo wa siasa zinazoendelea nchini ambazo zimewavuta wasanii wengi kujihusisha nazo wakiwa kama chachu ya ushawishi katika upande wanaousapoti.

Joh amesema kuwa yeye katika siasa hizo ni kama mwananchi wa kawaida na kwamba kila mtu ana haki ya kufanya maamuzi yake.

“Neno langu sio sheria, kwahiyo mtu anaeenda kufanya show kaona hiyo ni njia ya kupata kipato au kutimiza hisia zake,” Joh aliiambia Planet Bongo ya East Africa Radio.

Aliongeza kuwa wasanii wanaofanya kampeni hivi sasa katika vyama vya siasa wasichukuliwe kama wanakosea kwa kuwa wao ni binadamu.

“Mwisho, hii ni demokrasia na kila mtu ana uwezo wa kuamua na kuonyesha mapenzi yake binafsi,” alisema.

Pacquiao Kuachana Na Masumbwi 2016
Diamond Aielezea Sura Ya Mwanae ‘Tiffah’