Inaelezwa kuwa wachezaji saba wa Simba SC hawatakuwa sehemu ya kikosi cha Klabu hiyo kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ASFC pamoja na Michuano ya Kimataifa.

Maamuzi ya kuachwa kwa wachezaji hao yamefikiwa kufuatia dhamira ya Benchi la Ufundi na Uongozi wa Simba SC ya kutaka kuona kikosi cha Klabu hiyo kikirejesha heshima ya kutwaa mataji katika Michuano ya ndani na kufika Nusu Fainali ama Fainali upande wa Kimataifa.

Msimu huu 2022/23, Simba SC imekosa makombe matano iliyoshindania ambayo ni Ngao ya Jamii, Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho la Tanznia Bara ‘ASAFC’, Kombe la Mapinduzi na Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Mmoja wa mabosi wa Simba, amesema haraka mabosi wa Simba SC wamefikia makubaliano ya kuachana na wachezaji tisa ambao ni Joash Onyango, Nassoro Kapama na Habib Kyombo.

Wengine ni Mohammed Ouattara, Jimmyson Mwanuke, Augustine Okrah, Nelson Okwa, Ismail Sawadogo na Victor Akpan, huku wengine wakijadiliwa akiwemo Erasto Nyoni na Peter Banda.

Amesema kati ya wachezaji watakaokutana na panga hilo, kati yao mikataba inamalizika mwishoni mwa msimu huu.

“Hakuna jinsi ni lazima tuachane na baadhi ya wachezaji ili tupate nafasi ya kusajili wengine watakaokiimarisha kikosi.

“Tayari yapo baadhi ya majina yaliyokabidhiwa kwa uongozi kutoka kwa Kocha Robertinho (Roberto Oliveira), kati ya hao tutakaoachana nao wapo wanaomaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu huu na wengine tunaivunja,” amesema kiongozi huyo

Baadhi ya Wachezaji wanaotajwa kuwepo katika mipango ya kusajiliwa na Simba SC msimu ujao ni beki wa kati wa Rayon Sports ya Rwanda, Abdul Rwatubyaye, kiungo wa Geita Gold, Edmund John na kipa wa Vipers FC ya Uganda, Alfred Mudekereza.

Akizungumzia hilo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema: “Lipo wazi, ni lazima baadhi ya wachezaji tuwape mkono wa kwa heri kwa maana ya kuachana nao mwishoni mwa msimu huu.

“Uongozi utakutana kumfanyia tathimini mchezaji mmoja mmoja kwa kuangalia kiwango chake na msaada wake katika timu ambao ameutoa msimu huu, tunataka kuwa na wachezaji wapya watakaotuvusha Nusu Fainali ya michuano ya Afrika, tumechoka kila msimu tunaishia Robo Fainali.”

Simba SC juzi Jumapili (Mei 07) ilifungwa mabao 2-1 na Azam FC, matokeo ambayo yamaifanya klabu hiyo katika hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’, mchezo uliopigwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.

Ikumbukwe kuwa, Simba iliweka nguvu zao katika michuano hiyo baada ya kutokuwa na nafasi ya kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara pamoja na kutolewa katika Robo Fainali, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Mikel Arteta: Bado tuna ndoto za ubingwa EPL
Waumini 25 Kanisa la Kibaptist watekwa nyara