Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis ameendelea na ziara yake ya kihistoria nchini Iraq ambapo ametoa wito kwa Viongozi na Watu wa Nchi hiyo kuepuka vurugu na mivutano ya kidini.
Papa Francis anafanya ziara ya siku nne nchini Iraq ambayo ni ya kwanza kufanywa na Kiongozi wa Kanisa Katoliki katika Nchi ya Iraq
Usalama umeimarishwa kwa ajili ya kumlinda Kiongozi huyo baada ya kutokea mashambulio ya roketi na yale ya kujitoa muhanga katika siku za hivi karibuni nchini humo.
Wakati huo huo hatua za kiafya zinazingatiwa zaidi kutokana na hali ya maambukizi ya virusi vya Corona yanayoongezeka Iraq.
Baba mtakatifu atakutana na Kiongozi wa Madhehebu ya Shia nchini Iraq, Ayatollah Ali Sistani na pia atatembelea miji minne ukiwemo mji wa Mosul ambako Makanisa na turathi nyingine zimeharibiwa na wanamgambo wa itikadi kali.