Nahodha na mshambuliaji wa kikosi cha Lupuli FC, huenda akaachana na klabu hiyo ya mkoani Iringa mwishoni mwa msimu huu, kufuatia mkataba wake kuwa ukingoni.

Mkataba wa Lipuli FC na mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu za Mbeya City, Mwadui FC na Young Africans unatazamiwa kufikia kikomo Juni Mosi mwaka huu, na baada ya hapo mshambuliaji huyo atakua huru kuelekea anakotaka.

Taarifa kutoka mkoani Iringa zinaeleza kuwa, Nonga ameshakutana na viongozi wa Lipuli FC kwa mazungumzo ya awali ya kusaini mkataba mpya, lakini hajaonyesha dalili za kukubali kufanya hivyo.

Hatua hiyo inaashiriwa wazi huenda Nonga akawa na mipango ya kuondoka klabuni hapo, na kujiunga na klabu nyingine kwa msimu ujao wa ligi kuu ya soka Tanzania bara.

Kwa mantiki hiyo viongozi wa Lipuli FC watalazimika kuanza mchakato wa kumsaka mbadala wa mshambuliaji huyo ili kuziba pengo lake.

Mpaka ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu huu wa 2019/20 inasimamishwa mwezi Mei, kupisha mapambano ya maambukizi dhidi ya virusi vya Corona, tayari Nonga alikua ameshaifungia Lupilu FC mabao 11 na kutoa assist 4.

Peneza aitaka Serikali iwasaidie wafanyabiashara walioathirika na COVID 19
Tete atamani kutua Hispania, England