Makamu mwenyekiti wa Juventus, Pavel Nedved amesisitiza kuwa Bayern Munich wanafungika ingawa alikuwa akitegemea timu nyepesi zaidi katika ratiba ya timu 16 bora za michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyopangwa leo.

Juventus ambao walitolewa na waliokuja kuwa mabingwa wa michuano hiyo msimu uliopita Barcelona, wamepangwa kucheza Bayern iliyo chini Pep Guardiola katika shughuli hiyo iliyofanyika jijini Nyon.

Bahati mbaya ya kupangwa na kigongo hicho imekuja kufuatia kushindwa kwao kufuzu kama vinara wa kundi D wakiwaacha Manchester City kuongoza.

Akihojiwa mara baada ya shughuli hiyo Nedved amesema ni kweli alikuwa akitegemea timu nyepesi zaidi lakini hakuna shaka kwani wanaweza kuwashangaza hata mabingwa hao wa Ujerumani.

Jiji La Roma Lapewa Heshima Ya Uenyeji Wa Ryder Cup
Azam FC Kufanya Mazoezi Kwa Njia Za Digitali