Wachezaji wa timu ya soka ya Azam wanazidi kuziacha mbali timu za Simba na Yanga kufuatia mazoezi yao kuongozwa na kompyuta.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kupitia ukurasa wao wa facebook wa klabu hiyo, kwa sasa mazoezi ya viungo maarufu kama gym yanaongozwa na kompyuta.

Mtaalam wa masuala ya viungo, Adrian Dobre alisema katika mazoezi hayo ya gym, kila mchezaji hufunga kifaa maalum kiunoni mwake chenye mfano wa mkanda na kisha kufanya mazoezi.

Mkanda huo huwa na uhusiano wa moja kwa moja na kompyuta pakato(laptop) ambapo kiwango cha mazoezi cha kila mchezaji huonekana kwa wakati mmoja.

Alisema kama mchezaji anaonyesha kiwango cha chini, kompyuta hiyo huonyesha, hivyo hulazimika kumuita na kumwambia aongeze juhudi ya mazoezi.

Vifaa kama hivyo vimekuwa vikitika zaidi katika nchi za Ulaya, lakini Azam imethubutu na kuanza kutumia njia za kisayansi.

 

 

 

Pavel Nedved Aivusha Juventus Ligi Ya mabingwa Barani Ulaya
Kubenea Afikishwa Mahakamani, Chadema watoa Tamko dhidi ya Uamuzi wa Makonda