Kikosi cha Mabingwa wa Soka Dunia Argentina, kimewasili nyumbani Buenos Aires mapema leo Jumanne (Desemba 20), na kupata mapokezi ya kishujaa kutoka kwa mashabiki wa mji huo.

Kikosi cha Argentina kiliwasili mjini Buenos Aires majira ya nane usiku kwa saa za Argentina sawa na saa mbili asubuhi kwa saaa za Afrika Mashariki.

Mashabiki Wanaume na Wanawake bila kujali muda wa usiku, walijipanga pembezoni mwa barabara za mji wa Buenos Aires, kwa ajili ya kupongeza Wachezaji wa Argentina, ambao juzi Jumapili (Desemba 18) walipambana na Ufaransa kwenye mchezo wa Fainali nchini Qatar.

Katika hali ya kushangaza Ndege iliyowabeba wachezaji wa Argentina, ilionekana ikiwa na picha maalum za baadhi ya wachezaji wa timu hiyo eneo la mkia.

Shughuli maalum ya kuwapongeza kwa pamoja Wachezaji wa Argentina wakiongozwa na Gwiji Lionel Messi zimepangwa kufanywa katika mnara wa Obelisk, saa tisa mchana kwa saa za nchini humo.

Katika hatua nyingine Serikali ya Argentina imetangaza rasmi kuwa leo Jumanne (Desemba 20) kuwa siku ya mapumziko ya kitaifa kwa ajili ya kusheherekea Kombe la Ubingwa wa Fainali za Kombe la Dunia lililowasili nchini humo usiku wa kuamkia leo.

Karim Benzema aachana na Ufaransa
Ukomo wa bei za gesi waafikiwa