Kikosi cha Simba SC kimeanza safari ya kuelekea Mkoani Kagera tayari kwa mchezo wa Mzunguuko wa 17 wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kegera Sugar, utakaopigwa keshokutwa Jumatano (Desemba 21), katika Uwanja wa Kaitaba.

Simba SC imeanza safari hiyo ikitokea jijini Mwanza ambako jana Jumapili (Desemba 18) ilikua na mchezo wa Mzunguuko wa 16 wa Ligi Kuu dhidi ya Geita Gold FC, katika Uwanja wa CCM Kirumba na kuibuka na ushindi wa mabao 5-0.

Kupitia Kurasa za Mitandao ya Kijamii za Simba SC, kikosi cha klabu hiyo kimeanza safari mapema leo Jumatatu (Desemba 19)asubuhi huku wachezaji wote wakionekana kuwa katika hali nzuri na yenye furaha.

Ushindi dhidi ya Geita Gold FC umeiwezesha Klabu hiyo ya Msimbazi kufikisha alama 37 zinazoiweka nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, ikitanguliwa na Young Afrika yenye alama 41, huku Azam FC yenye alama 36 imeporomoka kwa nafasi moja hadi nafasi ya tatu.

Zahra Michuzi: Simba SC imetufunza jambo
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Desemba 19, 2022