Nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania *Taifa Stars* Mbwana Samatta amethibitishwa kuwa mchezaji mpya wa klabu ya Fenerbahce ya Uturuki.
Samatta amethibitishwa na kutambulishwa na uongozi wa klabu hiyo leo asubuhi kwa saa za Afrika mashariki, huku taarifa zikieleza amesaini mkataba wa miaka minne.
Mshambuliaji huyo anaanza maisha mapya nchini Uturuki, akitokea klabu ya Aston Villa inayoshiriki Ligi Kuu England (EPL), huku ikifahamika changamoto ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza, ndiyo sababu iliyomng’oa kwenye klabu hiyo ya mjini Birmingham.
Alisajiliwa na Aston Villa mwezi Januari 2020 akitokea KRC Genk ya Ubelgiji na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kucheza Ligi Kuu England (EPL).
Samatta ameondoka Aston Villa, hukua kiacha kumbukumbu ya kufunga mabao mawili.