Meneja wa uwanja wa Highland Estates uliopo Ubaruku Wilayani Mbarali mkoani Mbeya Malule Omary amesema uwanja unapaswa kutunzwa kwa muda wote ili uweze kukidhi vigezo vya kikanuni.

Uwanja wa Highland Estates unatumiwa na klabu ya Ihefu (Wana Mbogo Maji) inayoshiriki Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, ambapo Meneja wa Uwanja huo amechukua tuzo ya Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi Januari 2023.

Malule amefichua siri ya kuwa kuwa ili uweze Uwanja kufikia malengo ya kuwa na Uwanja bora unapaswa kuufanyia marekebisho mara kwa mara, kwa muda unapokuwa na changamoto.

“Uwanja unatunzwa sana huu, unajua Uwanja unahitaji maji mengi, sehemu ya kuchezea (pitch) inapaswa kutunzwa,”

“Sisi hapa tuna maji ya kutosha tuna kisima, tuna mabwawa ambayo yanarahisisha kazi, nawashukuru sana viongozi kwa ushirikiano” amesema Malule

Vifo tetemeko la ardhi Uturuki, Syria vyafikia 16,000
Serikali kuendeleza udhibiti matumizi mabaya mali ya umma