Mamlaka ya kudhibiti Mawasiliano Tanzania (TCRA) imempa onyo mwanamitindo na mjasiliamali Hamissa Mobetto kwa kukiuka maadili ya mtanzania na kuvunja sheria za mtandaoni kwa kurusha picha za utupu kupitia mtandao wa instagram.

Picha hizo zimekiuka maadili ya kitanzani na kushawishi watoto kuiga tabia mbaya ni zile zilizochapishwa tarehe 23 juni 2018 na traehe 10 Aprili  2018 ikionesha mama mjamzito akiwa ameshika tumbo lake juu kidogo ya sehemu za siri.

Aidha sheria inasema mtumiaji wa mtandao anatakiwa kuwajibika kwa maudhui anayoyaweka mtandaoni.

Hata hivyo Hamisa katika utetezi wake amekiri kuwa picha ni za kwake licha ya kukana kuwa hafahamu akaunti zilizotumiwa kuchapisha na kurusha picha hizo.

Kamati ya maudhui imesema kuwa kwakuwa Hamisa amekiri kuwa picha ni zake na alizipiga kwa lengo la kufanya biashara atawajibishwa.

Hivyo kamati imeamua kumpa onyo kali Hamisa Mobetto na endapo atatenda kosa kama hilo tena hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Pia kamati imemtaka Hamisa Mobetto kuomba radhi na kuweka tangazo kwenye akaunti yake ya instagram ili kuwaeleimisha mashabiki zake juu ya utumiaji wa picha zake zisizo za maadili.

Aidha TCRA imempa uwanja wa siku 21 kukata rufaa endapo ataona ameonewa juu ya tuhuma hizo zinazomkabili.

 

 

Alphonse Areola kumpisha Gianluigi Donnarumma PSG
Mohamed Salah aponda raha fukwe za Panama