Jeshi la Polisi Tanzania linatarajia kumuaga rasmi aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Mstaafu Balozi Simon Nyakoro Sirro, tarehe 10 Mei 2023 baada ya kustaafu Utumishi ndani ya Jeshi la Polisi kwa mujibu wa sheria mwezi Machi 2023.

Sherehe za kumuaga IGP Mstaafu Balozi Simon Nyakoro Sirro zitafanyika katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam kuanzia saa moja asubuhi kwa gwaride maalum la kumuaga ikiwa ni utaratibu wa Jeshi la Polisi kuwaaga kwa gwaride maalum viongozi wa Polisi waliofikia cheo cha Kamishna wa Polisi na Inspekta Jenerali wa Polisi.

IGP Mstaafu Balozi Siman Nyakoro Sirro amelitumika Jeshi la Polisi kwa miaka 30 tangu tarehe 19 Februari 1993 alipojiunga rasmi hadi kustaafu mwezi Machi, 2023 na ni Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Kumi (10) kuliongoza Jeshi la Polisi tangu uhuru.

Sirro ameliongoza Jeshi hilo kuanzia Mei 28, 2017 hadi Julai 20, 2022 na kupata mafanikio makubwa kwenye mapambano dhidi ya uhalifu na wahalifu ikiwemo kukomesha vitendo vya mauaji yaliyokuwa yakitokea wilayani Kibiti na maeneo mengine pamoja na kupunguza uhalifu nchini.

Wakuu wa Jeshi la Polisi waliomtangulia ni wafuatao na miaka waliyoongoza kwenye mabano; IGP mstaafu Elangwa Shaidi ambaye ni IGP wa kwanza tangu uhuru aliyaliongoza Joshi La Polisi Tanzania kuanzia mwaka 1964 hadi mwaka 1970, IGP mstaafu Hamza Azizi (1970-1973).

Wengine ni IGP mstaafu Samweli Pundugu (1973-1975), IGP Mstaafu Philemon Mgaya (1975 – 1980), IGP Mstaafu Solomon Lian (1980-1984), IGP Mstaafu Harun Mahundi (1984-1996) IGP Mstaafu Omani Mahita (1996-2006), IGP mstaafu Saidi Mwema (2006-2013), na IGP Mstaafu Emest Mangu (2013-2017).

Mafuriko DRC: Idadi ya vifo yafikia zaidi ya watu 500
UNFPA yaendeleza mapambano kufikia 0% vifo vya wajawazito