Idadi ya vifo nchini DRC imefikia zadi ya watu mia tano kutokana na mafuriko na kufunikwa na maporomoko ya matope yaliyosababishwa na mvua kubwa za siku nne mfululizo, huko Nyamukubi Wilayani Kalehe jimbo la Kivu kusini.

Mvua hizo, pia zimesababisha uharibifu wa nyumba, na kufanya maafa makubwa kuwahi kutokea katika historia ya hivi karibuni huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Hata hivyo, Wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu wamesema bado wanaendelea kutafuta miili zaidi ili kuweza kuwahifadhi katika makaburi mapya ya halaiki yaliyochimbwa mwishoni mwa wiki.

Wamesema, wametumia siku kadhaa kuopoa miili katika vijiji vya Bushushu na Nyamukubi vilivyopo katika mkoa wa Kivu Kusini, ambako mvua kubwa ya siku kadhaa ilisababisha maporomoko ya udongo na mito kuvunja kingo.

Apata Utajiri kwa Kucheza Aviator ya Meridianbet
Polisi kumuaga rasmi IGP mstaafu, Balozi Simon Sirro