Polisi mmoja Wilayani Sikonge Mkoani Tabora amewekwa chini ya ulinzi mara baada ya kumtolea maneno ya kejeli mwananchi huku akimhusisha Mkuu wa Wilaya hiyo mapema mwezi April mwaka huu.

Uamuzi huo umetolewa mjini Sikonge na Mkuu wa Mkoa wa Tabora,  Aggrey Mwanri baada ya Mkazi mmoja wa Sikonge Hidaya Hussein kumweleza kiongozi huyo wakati akisikiliza kero mbalimbali za wananchi.

Mkazi huyo amesema kuwa mnamo Aprili 26 mwaka huu alitoka kwake kwenda kuangalia katika kibanda kuangalia Sherehe za Muungano kwenye runinga na aliporejea alikuta Polisi wamevunja mlango wake na kuingia ndani ya nyumba yake bila ya yeye kuwepo na kupekua bila kuona kitu kibaya.

Aidha, mkazi huyo alinukuu baadhi ya maneno aliyomtamkiwa na polisi huyo  “Ulitaka kwenda kwa Mkuu wa Wilaya kushitaki, unadhani tunamuogopa Mkuu wa Wilaya kwanza hujui na wewe tunaweza kukuwekea bangi kisha tukukamate,”amesema Hidaya.

Hata hivyo, amemuagiza Mkuu wa Polisi Wilaya kumtafuta Polisi aliyetoa lugha hiyo na kumchukulia hatua na kuongeza kuwa kwa sababu mwananchi anamjua mhusika gwaride la utambuzi lifanyike.

 

Sentensi 10 za JPM baada ya kupokea ripoti ya uchunguzi wa Tanzanite, Almasi (+Video)
Kijana aliyeteka watoto Arusha afariki dunia