1. “Nyinyi (kamati) mmehatarisha maisha yenu, mngeweza hata kupewa sumu, lakini mmetanguliza utanzania”
  2. “Huu ulikuwa mtego, kama hizi ripoti zingekuwa za juu juu ningeunda ya kwangu ya wataalamu”
  3. “Nimesikia wengine wanasema wanapunguza wafanyakazi, mimi nilitamani kusikia wameondoka”
  4. “Wote waliotajwa kwenye ripoti ambao ni wateule wangu, ni matumaini yangu watakaa pembeni’
  5. “Nakubaliana na wewe kuwa mtaandika barua kwenye vyama vinavyohusika kuhusu wabunge wanaotajwatajwa”
  6. “Hii ripoti inanipa mwanya hata kuangalia hata jinsi ya kuwa nachagua wasaidizi wangu”
  7. “Aliyevumbua hayo mabaya ni Prof. Mruma, ndiye aliyefanya hadi tukafahamu ni Prof. Mruma”
  8. “Uhuru wa kweli ni uchumi ambao utalisha watoto wako, utatengeneza barabara na kuendesha nchi kwa manufaa ya wote
  9. “Wapo Watanzania ambao ni wazalendo sana, ndio maana hao wazungu wa dhahabu wapo hadi leo wanazungumza”
  10. “Nchi yetu imechezewa sana, na hao wanaotuchezea sijui kama wanatuona sisi ni binadamu au majitu”

JPM awakaanga waliotajwa kwenye ripoti ya madini
Polisi matatani kwa kumtolea lugha chafu mwananchi