Mkuu wa kikosi cha usalama Barabarani Mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi, SP Solomon Mwangilo amewataka madereva wa vyombo vya moto kuwa makini na matumizi ya vyombo hivyo ikiwemo kufuata sheria za usalama barabarani, ili kuepusha ajali za mara kwa mara.
Mwangilo ameyasema hayo ayo yamesema hii leo Novemba 8, 2022 wakati wa kukabidhi pikipiki kwa viongozi wa dini Mkoa wa Manyara, Kilimanjaro na Arusha na kusema kuwa viongozi hao wanawajibu
wa kutibu mioyo ya wanadamu kiroho ikiwemo kuwa makini na matumizi ya vyombo vya moto.
Amesema, Jeshi la Polisi pia lina wajibu kutoa Elimu kwa makundi yote ili kuwa na uelewa wa pamoja kwa minajili ya kukomesha ajali katika mkoa wa wa Arusha huku akiwataka madereva wa vyombo vya moto maarufu wanaofanya safari zao nje ya jiji la Arusha kufanya marekebisho ya vyombo hivyo.
Awali, Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) DkT. Barnabas Mtokambali alisema lengo la kutoa vyombo hivyo ni kuwafikia waamini, kutoa huduma ya kiroho, kazi za kanisa, na kuongeza kasi ya maendeleo.