Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa, ametoa onyo kali kwa mamlaka za maji na usafi wa mazingira nchini kuacha tabia ya kuwabambikizia bei za ankara za maji wateja.

Ameyasema hayo jijini Dodoma alipokuwa akifungua kikao kazi cha siku mbili kwa watendaji wa mamlaka za maji za mikoa na wilaya.

Prof. Mbarawa ametoa onyo hilo kwa wakuu wa mamlaka hizo ambao bado wanatoza gharama za huduma kwa wateja (Services Charges) kuacha mara moja kwani atakaye bainika mshahara wake utakatwa ili kurejesha fedha za wateja.

“Tusiwabambikizie wateja wetu bili za maji kiasi ambacho hawajatumia, wananchi wamekuwa wakilalamika  katika maeneo ambayo nimekuwa nikipita kuzungumza nao nawataka watendaji wote kuacha mara moja tabia hii”amesema Prof. Mbarawa.

Aidha, amesema kuwa amekuwa akipokea malalamiko mengi kutoka kwa wateja kubambikiziwa ankara za maji na mamlaka za maji katika maeneo mbalimbali nchini.

Hata hivyo amezungumzia juu ya malipo ya gharama za huduma ambapo amezitaka mamlaka zote za maji nchini kuacha kutoza wanachi na atakae bainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

 

Watoto wa Uganda waonesha jumba walilonunuliwa na French Montana
Theophilus Afelokhai achukua nafasi ya Francis Uzoho Super Eagles