Mwenyekiti wa Chama Cha wananchi CUF Profesa Ibrahimu Lipumba leo Jumanne Agust 11 – 2020, amechukua fomu za kuwania nafasi ya Urais kupitia Uchaguzi Mkuu, utakaofanyika mwezi Oktoba.
Lipumba amechukua fomu hizo katika ofisi za NEC mjini Dodoma, akiongozana na mgombea mweza wa chama hicho Hamida Huwesh.
Bada ya kuchukua fomu kwenye ofisi za NEC, Prof. Lipumba alisema Chama cha CUF msingi wake na itikadi ni HAKI SAWA KWA WOTE, hivyo atahakikisha wanatekeleza madhumuni ya chama endapo watachaguliwa na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na kuliwezesha taifa kuwa na dira moja.
Aidha ameongoza kuwa chama cha CUF kimejikita katika kutengeneza uchumi kukua kwa kasi na kuongeza ajira na kutokomeza umaskini ili kuendana na malengo ya kimataifa ya kumaliza umasikini ifikapo mwaka 2030.
Ameongeza kuwa chama cha CUF kitaboresha sekta elimu na sekta ya afya hasa katika upande wa upungufu wa damu kwenye kitengo cha mama mjamzito.
Katika hatua nyingine Prof. Lipumba, ameongeza kuwa kampeni za chama cha CUF zitaandia mjini Dodoma, kwa mujibu wa ratiba ya chama hicho.