Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba jana alizua taharuki kwa wanachama wa chama hicho baada ya kutaka kuzungumza na vyombo vya habari wakati ambapo kuna taarifa kuwa ana mpango wa kujiuzulu nafasi hiyo.

Wananchi wa chama hicho walivamia ofisi za makao makuu ya chama hicho katika eneo la Buguruni, Dar es Salaam kwa lengo la kumzuia asizungumze na vyombo vya habari kwanza hadi pale lengo lake litakapofahamika.

Muda mfupi baadae, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Tanzania Bara, Magdalena Sakaya alizungumza na vyombo vya habari na kueleza kuwa Profesa Lipumba amelazimika kuahirisha kuongea na wana habari hadi hapo baadae watakapofahamishwa tena. Alisema viongozi na wazee wa chama hicho walikuwa katika makao makuu hayo, wamemzuia na kuanza kuzungumza nae.

Wanachama wa CUF na waandishi wa habari wakimsumbiri Prof. Lipumba

Wanachama wa CUF na waandishi wa habari wakimsumbiri Prof. Lipumba

Baada ya mazungumzo hayo, Profesa Lipumba alijitokeza mbele ya waandishi wa habari na mamia ya wanachama hao walimpokea kwa furaha wakiwa na kiu ya kusikia neno kutoka kwake.

Prosesa aliwaondoa wasiwasi wanachama hao kuwa hana mpango wa kujiuzulu kama ilivyoripotiwa. Lakini akatoa kauli zilizoonesha kuwa kuna hali ya mtafaruku kati yake na viongozi wenzake.

“Katiba ya chama chetu imempa kila mwanachama haki na wajibu wa kujenga chama chake, kwa hiyo kujenga chama hakitegemei wadhifa alionao. Nilipopewa ridhaa ya kugombea urais tangu mwaka 1995 nilifanya hivyo ingawa kulikuwa na wanachama wa kawaida na waasisi. Chama ni taasisi na sio mali ya mtu binafsi,” alisema Lipumba.

Taarifa zisizo rasmi kutoka ndani ya chama hicho zinaeleza kuwa Profesa Lipumba amekuwa katika wakati mgumu baada ya kutofautiana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad.

Hata hivyo, taarifa hizo zilikanushwa na Maalim Seif wakati akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Chadema uliofanyika mapema wiki hii.

Sturridge Uso Kwa Uso Na Man Utd Septemba 12
West Ham Utd Warejesha Mashambulizi Kwa Chicharito