Wanafunzi 184 wa shule za msingi na sekondari mkoani pwani wamekatisha masomo kwa mwaka 2019 kutokana na kupata mimba kwa mwaka 2019.

Kati ya wanafunzi hao waliopata ujauzito, wa shule za msingi ni 40 na 144 wa sekondari, huku wanafunzi 1,907 wakishindwa kuendelea na masomo kutokana na utoro.

Kutokana na janga hilo, mkuu wa mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo amewaagiza wakaguzi wa shule kufuatilia maendeleo ya elimu mara kwa mara.

Amesema wakaguzi hao wanatakiwa kufuatilia ufundishaji wa walimu, utoro na hali ya chakula cha mchana ambavyo ni vikwazo vinavyochochea utoro.

Takwimu hizo zimetolewa na ofisa elimu wa mkoa wa Pwani, Abdul Maulid mjini Kibaha wakati wa kikao cha wadau wa elimu.

” Utoro ni moja ya vikwazo katika suala la elimu katika mkoa wetu, wengine ni umbali mrefu kutoka nyumbani na ilipo shule na wanafunzi kutopata chakula shuleni” amesema Maulid.

Pia amebainisha kuwa wanafunzi 2,221 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu, hawajaripoti shuleni hadi sasa na hawajulikani waliko.

Baada ya kupewa takwimu hizo RC Ndikilo ametoa agizo kwa kila halmashauri kufanya juhudi za kuwasaka wanafunzi ambao hawajaripoti shuleni hadi sasa na kufika shuleni kabla ya Machi 30.

“Kila mwaka tuna kikao cha wadau, lakini sijawahi kuona taarifa za hatua zilizochukuliwa kwa wanaowapatia wanafunzi mimba, tunataka tuone nini kinafanyika kwa wahusika ili tabia hii ikomeshwe na tuondokane na hili katika mkoa wetu” Ameagiza DCNdikilo.

Kikao hicho kilihudhuliwa na wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, baadhi ya wakuu wa shule, maofisa elimu na wadau wa elimu.

China: Serikali yapiga marufuku ulaji wa popo, Nyoka, kuzuia Corona
Rushwa yamtia mbaroni Askari Mgambo