Waamuzi wa 36 kutoka Mataifa 31 wameteuliwa kuchezesha Michezo ya Fainali za Kombe la Dunia 2022, zitakazoanza kurindima Jumapili (Novemba 20) nchini QATAR.
Shirikisho la Soka Duniani kupitia Kamati yake ya Waamuzi imetoa orodha hiyo na kwa mara ya kwanza Michezo ya Fainali hizo itachezeshwa na Waamuzi Wakike.
Waamuzi Wanawake waliotajwa kwenye orodha hiyo wapo Sita, watatu ni Waamuzi wa Kati na wengine Watatu ni waamuzi wasaidizi.
Katika hao mwamuzi mmoja anatokea Afrika Mashariki, nchini Rwanda, Salima Mukansanga mwenye umri wa miaka 34.
Waamuzi wengine ni Yoshimu Yamashita kutoka Japan na Stephanie Frappart kutoka Ufaransa.
Mwaka huu 2022 Salima Mukansanga aliweka historia ya kuwa Mwanamke wa Kwanza kuchezesha Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2021’ zilizopigwa nchini Cameroon.
Orodha ya Waamuzi 36 iliyotajwa na Kamati ya Waamuzi ya Shirikisho la Soka Duniani ‘FIFA’: Ivan Barton (Slovenia), Chris Beath (Australia), Raphael Claus (Brazil), Matthew Conger (New Zealand), Ismail Elfath (Marekani), Mario Escobar (Guatemala), Alireza Faghani (Iran) na Stephanie Frappart (Ufaransa).
Wengine ni Bakary Gassama (Gambia), Mustapha Ghorbal (Algeria), Victor Gomes (Afrika Kusini), Istvan Kovacs (Romania), Ning Ma (China), Danny Makkelie (Uholanzi), Szymon Marciniak (Poland), Antonio Mateu (Hispania), Andres Matias Matonte Cabrera (Uruguay) na Mohammed Abdulla Mohammed (Falme za Kiarabu).
Pia yupo Salima Mukansanga (Rwanda), Maguette N’Diaye (Senegal), Michael Oliver (England), Daniele Orsato (Italy), Kevin Ortega (Peru), Cesar Ramos (Mexico), Fernando Rapallini (Argentina), Wilton Sampaio (Brazil), Daniel Siebert (Ujerumani), Janny Sikazwe (Zambia), Anthony Taylor (England), Facundo Tello (Argentina), Clement Turpin (Ufaransa) na Jesus Valenzuela (Venezuela).