Kocha wa Timu ya Taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps amemuita mshambuliaji Randal Kolo Muani anakipiga katika klabu ya Eintracht Frankfurt ya Ujerumani, kuchukua nafasi ya Christopher Nkunku.

Nkunku aliondolewa kikosini mapema jana Jumatano (Novemba 16), baada ya kupata jeraha la mguu akiwa kwenye mzoezi ya mwisho kabla ya kuanza safari ya kuelekea QATAR.

Nkunku mwenye umri wa miaka 25 alipata jeraha jana Jumanne alipogongana na mchezaji wa Real Madrid, Eduardo Camavinga.

Randal Kolo Muani ameanza vyema sana msimu huu, ambapo mpaka sasa amefunga magoli matano (5), asisti 9 katika michezo 14 alizocheza katika Ligi Kuu ya Ujerumani ‘Bundesliga’.

Tayari kikosi cha Ufaransa kimeshawasili QATAR kwa ajili ya kutetea ubingwa wake, kikitarajia kuanza kufanya hivyo Novemba 22 kwa kucheza dhidi ya Australia katika Uwanja wa Al Janoub, uliopo mjini Al Wakrah.

Mchezo wa pili Ufaransa itacheza dhidi ya Denmark Novemba 26 mjini Doha katika Uwanja wa 974 na itamaliza Michezo ya Hatua ya Makundi kwa kupapatuana na Tunisia Novemba 30 mjini Al Rayyan kwenye Uwanja wa Education City.

Kenya yaondoa marufuku uagizaji GMO
Kocha Mgunda atoa pongezi Simba SC