Mabingwa wa soka barani Ulaya Real Madrid, wanajiandaa kumsajili kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa na klabu ya Newcastle Utd ya nchini England, Moussa Sissoko.

Real Madrid wameripotiwa kutenga kiasi cha Euro milion 30, kwa ajili ya kukamilisha dili la usajili wa kiungo huyo, ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa wakati wa fainali za Euro 2016.

Sissoko ameshaonyesha nia ya kutaka kuachana na Newcastle Utd, tangu mwishoni mwa msimu uliopita, na tayari meneja wa The Magpies Rafa Benitez ameshakubaliana na matakwa ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26.

“Wakati mwingine inakua vigumu kuendelea kuwa na mchezaji ambaye ameshaonyesha nia ya kutaka kuondoka,” Alisema Benitez alipohojiwa na BBC Sport.

“Tunajaribu kuzungumza nae kwa sasa, lakini bado Moussa Sissoko anaonyesha kuwa katika hali ya kutoridhishwa na mazingira ya Newcastle Utd, hivyo hatuna budi kukubali kumuachia na kwenda kujiunga na klabu anayoipenda.” Aliongeza Benitez

Moussa Sissoko, alisajiliwa na NewcstleUtd mwaka 2013 akitokea nchini kwao Ufaransa alipokua akiitumikia klabu ya Toulouse.

CUF wadai wanasubiri Maalim Seif akamatwe, kurejea leo
Rio Ferdinand Amtahadharisha Paul Pogba