Wagombea kumi na mbili ikiwa ni pamoja na wanawake watatu jana Desemba 5, 2020 wamehitimisha siku ya mwisho ya kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge.

Wagombea wanaoongoza zaidi katika uchaguzi utakaofanywa kesho Jumatatu ni Rais Nana Akufo-Addo anayewania muhula wa pili madarakani, na rais wa zamani John Mahama.

Hii ni mara ya tatu kwa viongozi hao wawili kuchuana katika uchaguzi, na hivyo ushindani mara hii unatarajiwa kuwa mkubwa.

Zaidi ya watu milioni 17 wameandikishwa kupiga kura katika uchaguzi wa nane wa taifa hilo tangu liliporudi katika siasa za kidemokrasia karibu miaka 30 iliyopita.

Matokeo yanaweza kuanza kutangazwa saa 24, baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa.

Mbegu ya Parachichi inavyosaidia kupunguza maumivu
ACT-Wazalendo yatoa sababu kuridhia Serikali ya Umoja wa Kitaifa