Raia wa Liberia wamepiga kura kumchagua mrithi rais Ellen Johnson Sirleaf ambaye ni mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa rais barani Afrika na mshidi wa tuzo ya amani ya Nobel.

George Weah aliyewahi kuwa mcheza soka bora duniani na makamu wa rais Joseph Boakai ndio wagombea wakuu kwenye kinyanganyiro hicho.

Rais wa sasa wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf amewashauri watu kupiga kura kwa amani kwenye taifa hilo ambalo bado linajijenga baada ya kutokea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka 14.

Jumla ya wagombea 20 wa urais akiwemo Alex Cummings mkurugenzi wa zamani wa kampuni ya Coca-Cola na MacDella, mwanamitindo na mpenzi wa zamani wa George Weah wanawania urais kumrithi Bi Sirleaf.

“Kura yako inakuhusu wewe na familia yako, sio chama wala kabila,” alisema Sirleafmwenye umri wa miaka 78 ambaye anaondoka madarakani baada kuongoza kwa mihula miwili.

Ellen Johnson Sirleaf aliingia madarakani mwaka 2006 baada ya Charles Taylor kulazimishwa kuondoka madarakani na waasi mwaka 2003, Taylor kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka 50 jela nchini Uingereza kwa makosa ya uhalifu wa kivita na mzozo katika nchi jirani ya Sierra Leone.

 

Karibu watu milini 2.2 wamejiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi huo wa urais unaofanyika leo. Uchaguzi wa bunge nao unafanyika leo.

Diwani amtaka Mbowe kumtafuta Dkt. Slaa
Iceland yaweka rekodi, ni nchi ndogo kuwahi kufuzu kombe la dunia