Mwanasheria Mkuu wa Serikali Kenya, Githu Muigai ameonya vikali hatua inayotaka kuchukuliwa na mpinzani wa Rais Kenyatta, Raila Odinga ya kutaka kujiapisha ifikapo tarehe 12, na kusema kuwa kwa kufanya hivyo atakuwa amevunja katiba ya nchi hiyo.

Aidha ameeleza kuwa akijaribu kujiapisha kama alivyopanga atashtakiwa kwa kosa la uhaini ambalo adhabu yake ni kifo, kutokana na kwenda kinyume na katiba kwani tayari Rais kwa kupitia tume ya uchaguzi amekwisha pitishwa na kuapishwa.

‘Kumuapisha mtu yeyeote ambaye hajatangazwa tume ya uchaguzi kuwa ameshinda uchaguzi na ambao hajasimiwa na Jaji Mkuu ni kinyume na Katiba na Uhaini wa hali ya juu’’ amesema Githu Muigai.

Pia mwanasheria huyo ameonya Kaunti 11 zilizopitisha mjadala wa Bunge la Watu na kusema wamevunja sheria na wanatumia vibaya pesa za walipa kodi.

Kiongozi huyo wa upinzani Raila Odinga alikataa kushiriki uchaguzi wa marudio ulioamriwa kufanyika tarehe 26 oktoba baada ya mahakama kuu kufuta matokeo ya uchaguzi  wa tarehe 8 Agosti akidai amejiondoa kuipisha tume ya uchaguzi IEBC muda wa kutosha kufanya mabadiliko ambayo yatawezesha kufanyika uchaguzi kwa njia ya haki.

Kwa awamu ya pili uchaguzi chini ya tume ya uchagzui Kenya ulifanyika Oktoba 26, na Rais Uhuru Kenyatta aliapishwa rasmi kuwa Rais nchini humo kwa awamu ya pili mnamo tarehe 28 Novemba.

 

Mambosasa aifumua upya kesi ya Dk Shika
Chanzo cha mwandishi kupotea chatajwa