Rais Cyril Ramaphosa amethibitisha rasmi kung’atuka kwa naibu wake, David Mabuza akimshukuru kwa uungwaji mkono wusioyumba katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Ramaphosa alikuwa mjini Cape, kwa ajili ya kujibu mjadala wa hotuba ya Taifa taarifa ambayo inakuja huku mabadiliko ya baraza la mawaziri yakitarajiwa katika wiki zijazo.

David Mabuza. Picha ya Bloomberg.

David Mabuza, alifichua mapema mwezi huu kuwa aliwasilisha ombi la kujiuzulu kwake na wapinzani wake walimshtumu kwa kuendesha kikundi kibinafsi kinachodaiwa kuwatisha wanasiasa wengine wakati akiongoza jimbo la kaskazini mashariki, Mpumalanga.

Nafasi ya naibu rais mpya, inatazamiwa kuzibwa na Paul Mashatile ambaye alichaguliwa wa chama tawala (African National Congress – ANC), kurithi nafasi ya David Mabuza.

Ramaphosa agoma AKA kufanyiwa mazishi ya kitaifa
Mchengerwa azindua magari 22 ya doria TAWA, ataka kazi