Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud amesema takribani watu 100 miongoni mwao wakiwa ni watoto wamefariki dunia na wengine 300 kujeruhiwa, baada ya kutokea kwa mlipuko wa mabomu mawili yaliyotegwa kwenye gari karibu na eneo lenye pilika nyingi la jirani na Ofisi za Wizara ya Elimu mjini Mogadishu.

Rais Mohamud ameyasema hayo hii leo Oktoba 30, 2022 na kusema Jeshi la Polisi liinachunguza tukio hilo ambalo linahusishwa na makundi ya kigaidi au watu wa kujitoa muhanga, huku mtumishi mmoja wa kituo cha tiba akisema wamepata miili ya watu 30.

Moshi ukiwa umetanda angani mjini Mogadishu katika eneo jirani na Ofisi za Wizara ya Elimu baada ya kutokea kwa mlipuko uliosababisha vifo vya watu 100 na kuwajeruhi wengine 300. Picha:  Abdihalim Bashir/ REUTERS.

Tuki hilo la kuhuzunisha la Jumamosi Oktoba 29, 2022 limetokea katika kipindi ambacho Rais, Waziri Mkuu na maofisa wengine waandamizi wa nchi hiyo wakiwa kwenye mkutano wa kujadili namna ya kukabiliana na kundi la al-Shabab ambalo mara nyingi limekuwa likiushambulia mji mkuu.

Aidha, mauaji hayo pia yanatokea katika kipindi cha takribani miaka mitano baada ya kutokea mripuko mwingine katika eneo hilo, uliogharimu maisha ya watu 500 na hadi sasa bado hakuna kundi lolote lililojitokeza kukiri kuhusika na shambulizi hilo.

Rais amtimua Balozi wa Rwanda akihofia usalama
Ukiacha kusoma unaacha kuongoza: Msigwa