Rais wa Zambia, Edgar Lungu amewaonya majaji nchini humo kutowaiga majaji wa Kenya waliotengua matokeo ya uchaguzi, hali iliyopelekea kufanyika uchaguzi wa marudio kitu ambacho amesema kitasababisha kuzuka kwa vurugu nchini humo.
Amesema kuwa majaji hao wa Kenya hawafai kuigwa kwani walitumbukiza nchi hiyo kwenye mzozo baada ya kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika Agosti ambapo Rais Kenyatta alikuwa ametangazwa kuwa mshindi.
Aidha, kumezuka mjadala mkali kuhusu Rais Lungu kama anafaa kuwania kiti hicho kwa muhula mwingine, huku wapinzani wakisema kuwa kwasasa anatumikia muhula wa pili na hivyo hawezi kuwania tena.
“Kwa wenzangu katika idara ya mahakama, ujumbe wangu kweni ni kwamba mfanye kazi yenu vizuri, mtafsiri sheria bila woga au kupendelea upande wowote na mzingatie maslahi ya nchi. Msiwe watu wa kuiga na mfikirie kwamba mtakuwa mashujaa iwapo mtatumbukiza nchi hii kwenye vurugu,”amesema Rais Lungu
-
Mpina awataka wafugaji kutembea kifua mbele
-
Halmashauri yasimamisha mishahara ya walimu 15
-
Ummy Mwalimu apiga marufuku biashara ya damu
Hata hivyo, wafuasi wa Rais Lungu wanasisitiza kuwa alimalizia muhula wa mtangulizi wake, hivyo muhula wake wa wa kwanza ulianza aliposhinda uchaguzi wa 2016, ambao ulikumbwa na utata