Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhanga Mpina  amewataka wafugaji nchini kutembea kifua mbele kwa kumpata yeye kama Waziri mwenye dhamana ya Mifugo,

Ameyasema hayo aliposhiriki zoezi la kupiga chapa Mifugo  katika Kijiji cha Kyelwa kilichopo katika kata ya Katerero Halimashauri ya wilaya Bukoba mkoani Kagera na kuwataka viongozi kuzingatia maadili wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo ili kuepuka hujuma na ubaguzi kwa wafugaji.

Mpina amewataka wafugaji hao kuendelea kujitokeza kwa wingi na kupeleka mifugo yao kupigwa chapa na kusema kuwa zoezi hilo ni la manufaa na faida kwa wafugaji kwani litaweza kuwasiadia kuhepuka maambukizi ya magonjwa ya wanyama kwa mifugo yao.

Aidha, kwa upande wake diwani wa kata ya Katerero, Nuru Abdul Kabendera amesema kuwa, amefurahishwa na ziara ya Waziri huyo katika kata ya katerero kwani ni mara ya kwanza kwa kata hiyo kupata ugeni kutoka katika ngazi ya juu ya serikali.

Hata hivyo, Mpina ameupongeza uongozi wa mkoa kwa oparesheni iliyofanyika ya kuondoa mifugo katika mapori tengefu na hifadhi za misitu.

TFF yatoa ufafanuzi wa malipo ASFC
35 waitwa kuunda kikosi cha U23