Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli, ameeleza ni namna gani alivyoshangazwa na mkulima alieshikilia ndege ya  ATCL kwa mamlaka ya Mahakama kuu ya Afrika Kusini, kwa kile alichokieleza ni wivu tu.

Rais Magufuli amesema hayo leo Septemba 16, 2019, katika uzinduzi wa Rada ya kuongozea ndege katika anga la Tanzania.

Ameeleza kuwa Shirika la Ndege la Tanzania linafanya vizuri na ndio maana kuna watu wanajitokeza kuishikilia.

Ndege ya kampuni ya ATCL ilikamatwa nchini Afrika Kusini Agosti 23, mwaka huu na iliachiwa Septemba 3, baada ya jopo la mawakili wa Serikali kwenda nchini humo na kushinda kesi.

”Shirika letu la ndege linaendelea vizuri, ndio maana mkisikia watu wanakamata ndege zetu msishangae sana hii ni kwa sababu ndege zetu zinafanya kazi vizuri, mimi huwa naona kama kelele za chura hazimzuii Ng’ombe kunywa maji” amesema Rais Magufuli.

 

Mabao ya Molinga 'Falcao' kununuliwa kwa mamilioni
Magufuli ampongeza Mtaturu kutwaa jimbo la Lissu