Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa ameendelea kuwapa nafasi ndani ya chama cha Zanu-PF na Serikalini vigogo wa Jeshi la nchi hiyo, ambapo wikendi alimteua kigogo wa zamani wajeshi, Constantino Chiwenga kuwa Makamu wa Rais wa chama hicho.
Mnangagwa pia amemtua katika nafasi hiyo mwanasiasa mkongwe, Kembo Mohadi hali inayowafanya wawili hao kuwa na nafasi ya kushika nyadhifa kama hizo ndani ya Serikali.
Mnangagwa ambaye alichukua nafasi ya Robert Mugabe aliyetawala nchi hiyo tangu ilipopata uhuru, ana changamoto ya kuhakikisha anarejesha hali nzuri ya uchumi na kuwavutia wawekezaji kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa taifa hilo.
Mugabe alilazimika kujiuzulu nafasi ya Urais baada ya Jeshi la nchi hiyo kuingilia kati mgogoro wa madaraka ndani ya ZANU-PF kwa kueleza kuwa linawasaka watu waovu waliomzunguka Mugabe na sio kumpindua.
- Tunisia yapiga marufuku ndege za Emirates kukanyaga ardhi yake
- Dkt. Shein awatahadharisha wanaodhani ni mpole
Mke wa Mugabe, Mama Grace alikuwa na mgogoro na Mnangagwa kwa muda mrefu, hali iliyopelekea Mugabe kumfukuza Mnangagwa na kumuondoa kwenye nafasi ya Makamu wa Rais.