Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali yake itaongeza fedha ya kujikimu kwa wanafunzi wa elimu ya juu kutoka sh. 8500 ya sasa hadi kufikia sh 10000.

Dkt. Samia ameyasema hayo wakati akijibu hoja mbalimbali zilizoibuliwa wakati wa mkutano wake na serikali za wanafunzi wa vyuo vikuu TAHLISO uliofanyika Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma.

Katika Mkutano huo Rais wa Shirikisho la Wananfunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania(TAHLISO) Frank Nkinda alimuomba Rais Samia kuongezewa fedha za kujikimu kutoka 0,500 za sasa hadi 10,000 kwasababu maisha yamepanda.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alipokutana na  viongozi wa Tahliso na Zahlife kwa upande wa Zanzibar, Ikulu jijini Dodoma.

Vilevile Nkinda alisema kwa sheria za sasa wanafunzi wanaosoma masomo ya ngazi ya cheti na stashahada si wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu hivyo akamuomba Rais kuwasaidia nao ili wabaufaike na mikopo.

Akijibu hoja hizo Rais Samia aliliridhia kkuongeza fedha za kujikimu kwa wanafunzi wa elimu ya juu ambapo alisema” Waziri wa Elimu elimu nenda kaangalie, tutaanza na sh 10,000″

Aidha alisema kuwa kuhusu wanafunzi wa cheti na stashahada kupata mikop hiyo jambo hilo halitawezekana kwa sasa ila wanaenda kujipanga na kuweka mipango ya kulitekeleza.

Kwa kazi tunazozifanya sasa hivi na hali ya bajeti badi hatujafika huko kwahiyo tunalifikilia tunaliweka kwenye mipango nilikuwa nanong’ona na Wazir wa elimu hapa nikamwabia nenda kajipekue vizuri ukiwa unaliweza niambie nami nipekue kwingineko kidogo nikujazie ili uwezo… kama tutashindwa mwaka huu, tuachieni tujipange mbele tutakenda nalo”amesema Rais Samia.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolph Mkenda

Naye Waziri wa Elimu Prof. Mkenda alisema wakati rais anaigia madarakani mikopo ya wanafunzi hao ilikuwa sh 464 bilioni ambapo alisema kuwa Rais Samia alielekeza wizara kufadhili masomo ya sayansi kwa wanafunzi wanaoanya vizuri na tayari wanafunzi 640 wamepata ufadhili huo.

“Kuna Scholarship zimetolewa pia kwaajili ya wahadhiri wa vyuo vikuu wakati wa kujadili mradi wa HIT maboresho ya taasisi za elimu ya juu uliangazi kujenga uwezo wa wahadhiri kwa kuwasomesha wengi zaidi, bilioni 2.3 zimetengwa kwa aajili ya wahadhiei kwenda kusoma kokote duniani” alisema Mkenda.

Mafuriko yaathiri familia 2,400
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Februari 12, 2023