Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa tuzo maalum ya juhudi zake za kuimarisha uhuru wa Habari na haki ya Wananchi kupata taarifa za kweli na sahihi.
Tuzo hiyo, imetolewa katika hafla ya ufunguzi wa kikao kazi cha Maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano Serikalini, kinachofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, tuzo hiyo iliyokabidhiwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye imepokelewa kwa niaba ya Rais na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Akiongea mara baada ya kukabidhi tuzo hiyo, Nape amesema, “tunatoa tuzo hii kwa kutambua mchango wa Rais katika kuhakikisha Watanzania wanakuwa na wigo mpana wa kupata taarifa za kweli na sahihi.”