Utawala wa kijeshi nchini Burkina Faso, umesitisha matangazo yote ya kituo cha televisheni cha Ufaransa France 24, katika nchi hiyo ya Afrika magharibi baada ya kituo hicho kufanya mahojiano na kiongozi wa kundi la Al-Qaeda.

Msemaji wa Utawala wa Kijeshi, Jean Emmanuel Ouedraogo amesema Serikali imeamua kusitisha mara moja matangazo ya vipindi vya France 24 nchini kote, msemaji alisema baada ya Kituo hicho kufanya mahojiano na kiongozi wa AQIM, Abu Ubaydah Yusuf al-Annabi.

Picha ya Alexander Klein/ Getty Images.

Amesema, “kwa kumpa nafasi kiongozi wa AQIM, France 24 haikufanya tu kitendo cha kuwa idara ya mawasiliano kwa magaidi hao lakini imehalalisha pia vitendo vya kigaidi na matamshi ya chuki.”

Burkina Faso, ambayo ilikumbwa na mapinduzi mawili ya kijeshi mwaka jana (2022), inapambana na uasi wa wanamgambo wa Kiislamu, ambao ulisambaa kutoka nchi jirani ya Mali mwaka 2015.

Rais Samia atunukiwa tuzo maalum uhuru wa Habari
Wenye silaha waharibu, wapora mali shamba la Rais Mstaafu