Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris ameachia rasmi orodha ya nyimbo 25 za wasanii anaowasikiliza zaidi kwenye mtandao wa Spotify kwa mwaka 2023, orodha ambayo imepewa jina la ‘Safari zangu’.

Orodha hiyo imetoka kufuatia ziara yake inayoendelea katika baadhi ya nchini za Afrika ikiwamo Tanzania, Ghana na Zambia, kwa kile kilichotajwa kama sehemu ya kuwapa hamasa wasanii wa muziki wa Afrika.

Mtandao wa Billboard umeichapisha orodha hiyo kwenye tovuti yao, kwa kusudio la kuwahamasisha wapenzi wa muziki ulimwenguni kusikiliza nyimbo za wasanii waliotajwa kupitia mitandao wa Spotfy pamoja na majukwaa mengine ya kusikiliza muziki online.

Miongoni mwa nyimbo na wasanii waliotajwa kwenye orodha hiyo kutoka nchini Tanzania ni pamoja na Alikiba ‘Mahaba’. Harmonize ‘Single Again’, Jux & Marioo ‘Nice Kiss’. Mbosso ‘Shetani’, Zuchu ‘Utaniua’, Darassa (No Body), Marioo & Abbah ‘Lonenly’, Platform & Marioo ‘Fall’. Jay Melody ‘Sawa’,.

Ziara ya Kamala tayari imeanza na mapema siku ya juzi aliwasili nchini Ghana na kufanya ziara yake yenye lengo la kugusa kwenye nyanja mbali mbali ikiwamo mabadiliko ya hali ya hewa (Climate change), pamoja na maendeleo ya kiuchumi, ambapo anatarajia kukutana na wasanii mbali mbali kutoka Barani Afrika.

Wawekezaji wa Kusini watua nchini, Wizara ya Madini yawapa neno
Rais Samia atunukiwa tuzo maalum uhuru wa Habari