Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini Tanzania ‘TPBRC’ Chaurembo Palasa amesema anaamini Bondia Hassan Mwakinyo ana nafasi kubwa kulipa kisasi dhidi ya Bondia Liam Smith wa England.
Mwakinyo alipoteza dhidi ya Smith Jumamosi (Septemba 03) kwa TKO mjini Liverpool, hali iliyozua taharuki kwa Mashabiki wake ambao walitarajia kuona akiibuka mshindi katika pambano hilo.
Palasa amesema baada ya Bondia huyo kutoka mjini Tanga kupoteza pambano hilo, amepata somo ambalo anaamini litamsaidia katika pambano lijalo.
“Naamini Mwakinyo kuna funzo amelipata baada ya kupoteza dhidi ya Smith, kuna vitu vingi amejifunza kwa sababu ukichaza ugenini dhidi ya Bondia mwenye uzoefu mkubwa kisha ukapoteza kuna kitu unajifunza.”
“Binafsi ninaamini Mwakinyo ana nafasi kubwa ya kurudisha hadhi yake ndani na nje ya Tanzania atakaporejea tena ulingoni, sina shaka na hilo kabisa.” amesema Palasa
Kupitia Ukursa wake wa Instagram Bondia Hassan Mwakinyo amethibitisha taarifa za kurudiwa kwa Pambano lake na Liam Smith mwezi Januari 2023.
Mwakinyo ameandika: Kutokana na mchezo wa jana na kitendo cha refa ree kuwa unfair kwangu kime mlazimu promoter @benjshalom kutupa nafasi ya rematch na Liam Januar2023??