Rais Kim Jong Un wa Korea ya Kaskazini amepiga marufuku kuimba, kunywa vileo na kufanya mikusanyiko ya aina yote nchini humo wakati wa Krismasi mwaka huu.
Wakati mwaka jana, Rais huyo aliwazuia Wakristo nchini humo kuadhimisha Krismasi na badala yake akawataka kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa bibi yake, Kim Jong-suk, aliyezaliwa siku ya mkesha wa Krismasi mwaka 1919.
“Korea ya Kaskazini imeanzisha mfumo wa jumuia za chama tawala kuripoti matatizo ya kiuchumi ya watu wanayokumbana nayo kila siku, na imepiga marufuku mikusanyiko inayohusiana na unywaji wa vileo, uimbaji na burudani nyingine, na imeimarisha udhibiti wa habari kutoka nje,” lilisema NIS.
-
Jafo atangaza shavu nono kwa walimu
-
NEC yashangazwa na mwenendo wa Chadema
-
Video: Dar24 yazindua rasmi kampeni ya Tupo Pamoja.
Fursa za kuitumia sikukuu hiyo kueneza uelewano na furaha zinazidi kufifia katika taifa hilo linalodaiwa kutawaliwa kidikteta na ambalo limepiga marufuku dini zote isipokuwa maadhimisho ya familia iliyoasisi taifa hilo la kikomunisti.
Miti yenye mapambo ya kuadhimisha Krismasi huonekana katika maduka makubwa ya bidhaa jijini Pyongyang, lakini kipindi hiki hakuna alama zozote za kidini.