Mkombozi wa Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Coastal Union Raizin Hafidh, amefunguka sababu za kushangilia mbele ya Benchi la timu ya Coastal Union, baada ya kufunga bao la kusawazisha.
Dodoma Jiji FC ilikuwa nyumbani juzi Jumapili (April 09) katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, huku ikitanguliwa kufungwa bao la mapema katika za kipindi cha pili, lakini Dakika ya 86 Raizin aliisaiwazishia timu hiyo 86 akimalizia pasi ya kiungo Muhsin Malima.
Bao la Coastal Union lilifungwa na mshambuliaji Maabad Maulid kwa kichwa akimalizia krosi ya kiungo Vicent Abubakari.
Raiszin ambaye aliwhi kuitumikia Coastal Union kabla ya kutimkia Dodoma Jiji FC alienda kwenye benchi la Coastal Union na kushangilia kwa nguvu, halia mbayo iliwastaajabisha mashabiki waliokuwa wakiufuatilia mchezo huo ulioanza mishale ya saa moja usiku.
“Kwanza ndio mechi yangu ya kwanza kuanza katika timu na kuaminiwa na Kocha, Melis (Medo) nimeichezea Coastal Union tangu U20 nimeshuka nayo na kupanda nayo.”
“Kuna kipindi kulikuwa na majungu nikaandika barua ya kuomba kuondoka tangu nimeondoka sijawahi kukutana nao ndio katika mchezo huu, nilisema siku moja nitakutana nao na nitawafunga nafurahi nimewafunga.”
“Nafurahi kwa sababu mimi miguu imeongea, Coastal naipenda na nimefunga mabao mengi sana nikiwa na timu ile, sijafurahi nilivyoondoka kwa majungu,” amesema mchezaji huyo.”
Kufuatia sare ya bao 1-1 Dodoma Jiji inashika nafasi ya 11 ikiwa na alama 28, huku Coastal ikiwa na alama 27 ikishika nafasi ya 12.