Rapa wa Marekani,Nipsey Hussle ameuawa kwa kupigwa risasi mapema leo nje ya duka lake la nguo lililoko Los Angeles.

Nipsey mwenye umri wa miaka 33, alipigwa risasi kadhaa mwilini mwake na alipofikishwa hospitalini alibainika tayari alikuwa ameshafariki, kwa mujibu wa CNN.

Watu kadhaa walijeruhiwa pia katika tukio hilo ambalo kwa mujibu wa polisi lilihusisha makundi mawili kushambuliana kwa risasi, Kusini mwa Los Angeles.

Nipsey alikuwa mmoja kati ya wakali wa rap waliotikisa ulimwengu mpya wa michano, ambapo albam yake ya ‘Victory Lap’ ilifanikiwa kutajwa kwenye kipengele cha albam bora ya rap/hiphop kwenye tuzo za Grammy mwaka huu, kipengele ambacho rapa wa kike Cardi B alifanikiwa kushinda na albam yake ‘Invasion of Privacy’.

“Hakuna mtu yeyote tunayemshikilia hadi sasa na tutatoa taarifa kadiri tutakavyozipata, uchunguzi wa tukio hili umeanza mara moja,” ameeleza Mkuu wa Idara ya Polisi ya Los Angeles.

Rihanna amekuwa mmoja kati ya wasanii wa kwanza wakubwa kumlilia rapa huyo kupitia mitandao ya kijamii, ambapo ameandika kwenye twitter jinsi alivyoshtushwa na taarifa hizo.

“Hii haileti maana yoyote! Roho yangu imetikishwa na hili! Mwenyezi Mungu, naomba ipumzishe kwa amani roho yake na ninaomba uwape faraja ya kiroho wapendwa wake wote! Ninasikitika sana hiki kimekutokea wewe @nipseyhhussle,” tafsiri ya ujumbe wa Rihanna.

Nipsey Hussle ambaye jina lake halisi ni Ermias Davidson,, alizaliwa Kusini mwa Los Angeles na aliwahi kuwa mwanafamilia wa kundi la kihalifu la Rollin’ 60 alipokuwa na umri mdogo.

Jana, alitweet ujumbe kuhusu kuwa na maadui, “kuwa na maadui imara ni baraka.”

 

Dudu Baya aipigia magoti familia ya Marehemu Ruge, Serikali ‘mnisamehe’
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Aprili 1, 2019