Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amepiga marufuku kwa viongozi wa Serikali kuwakamata watumishi wa umma na kuwaweka rumande bila kufuata sheria na taratibu za utumishi wa umma.
Amesema kuwa siku za hivi karibuni kumejitokeza tabia ya baadhi ya viongozi kuwakamata na kuwaweka rumande watendaji wa serikali bila kufuata sheria na taratibu za utumishi wa umma.
“Kama mtendaji alikosea kuna taratibu za kufuata, kuna masuala ya kiutumishi, kuna masuala ya kijinai na kiuchunguzi hivyo ni vyema yakafuatwa, lakini si kukurupuka tu na kuwaweka rumande,”amesema Gambo
Aidha, Gambo amewataka viongozi kutumia vyombo vilivyowekwa na serikali kutatua matatizo ikiwemo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) pia kufuata sheria za utumishi wa umma.
-
Watu 20 washikiliwa na polisi kwa tuhuma za ushoga
-
Nyumba yamtia matatani Zitto Kabwe
-
Watu wasiojulikana wamvamia Dereva wa Mbunge
Hata hivyo, amewataka watumishi wa umma kufanyakazi kwa kushirikiana na kuepuka majungu kwakuwa wote wanawatumikia wananchi hivyo wanatakiwa kutimiza wajibu wao kikamilifu.