Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi, Robert Luhumbi ameagiza kukaguliwa kwa mapato na matumizi ndani ya Kata ya Mgusu iliyopo kwenye Halmashauri ya wilaya ya Geita mkoani humo.

Luhumbi ametoa agizo hilo kwa  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita Mhandisi Modest Apolinary akimtaka apeleka wakaguzi wa ndani wa Hesabu za Serikali kwenye kata hiyo ya Mgusu ili wakakague na kujiridhisha,

“Mkurugenzi leta timu ya ukaguzi wa hesabu za Serikali ili ikague na kujiridhisha kama kuna fedha yoyote iliyochukuliwa pasipo maelezo yanayojitosheleza, hatua zichukuliwe haraka kwa wote watakaobainika kuhusika”, amesema Luhumbi

Aidha, Mkuu huyo wa mkoa yupo kwenye ziara yake mjini Geita akizindua kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na Zahanati ambapo amepokea malalamiko ya wakazi wa Machinjioni katika kata ya Mgusu waliodai kutosomewa taarifa za mapato na matumizi ya fedha zao.

Hata hivyo, Luhumbika ameongeza kuwa ukaguzi huo ufanyike kuanzia mwaka 2014 hadi 2017 kisha apate taarifa hiyo ofisini, na ameunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa na wananchi katika kujiletea maendeleo sambamba na huduma za jamii.

 

Tanesco: Upungufu wa umeme baadhi ya maeneo, jumamosi Novemba 18 na kesho Jumapili Novemba 19, 2017
Bombardier pasua kichwa Canada