Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Stephen Kagaigai amekemea vikali kwa Halmashauri kutokupeleka mapato ya asilimia 10 kwenye mfuko wa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.
Ameyasema hayo kufuatia uwepo wa hoja ya Halmashauri ya Wilaya ya Rombo na kupeleka pungufu ya asilimia 10 ya mapato ya ndani katika mfuko wa vijana, wanawake na wenye ulemavu katika kipindi cha mwaka 2019/2020.
Aidha RC Kagaigai amezitaka Halmashauri za Mkoa huo kuhakikisha zinatoa asilimia 10 ya mapato ya ndani ya vijana, wanawake na wenye ulemavu kwa wakati ili kuinua kipato na kuziletea halmashauri maendeleo.
RC Kagaigai Amesema ni muhimu Halmashauri kutoa fedha hizo kwa vijana ili wajikwamue kimaiha na kujipatia kipato ktika kuendeleza ujenzi wa Taifa
Amesema kuna taarifa za vijana wengi wilayani Rombo kujihusisha na vitendo vya unywaji wa pombe badala ya kufanyakazi za maendeleo.
Kanuni namba 5.5 [1] ya sera ya mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na wenye ulemavu iliyofanyiwa mabadiliko mwaka 2019 inataka kila halmashauri kuchangia asilimia 10 ya mapato ya ndani.