Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amewataka Watumishi kukopa kwa malengo ya kuboresha maisha ya sasa na baadae na kuhakikisha mikopo wanayochukua wanaitumia kuanzisha miradi yenye tija.
RC Makalla ametoa rai hiyo wakati akizungumza katika katika ufunguzi wa Semina ya Siku ya Walimu iliyoandaliwa na benki ya NMB.
Amewataka Walimu kuacha kurubuniwa kwa mikopo ya haraka ‘Chapchap’ yenye riba kubwa ambayo mwisho wa siku inawaingiza katika maisha magumu badala ya neema.
Aidha, RC Makalla amewapatia Walimu somo la namna Bora ya kutumia mshahara wao na kuweka akiba kwa ajili ya kuanzisha miradi ya kujiimarisha kiuchumi ili watakapostaafu waweze kuishi maisha bora, “Mshahara wako ni sawasawa na matumizi na kujiwekea akiba.”