Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limetangaza donge nono la kiasi cha shilingi milioni mbili kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa kwa jeshi hilo kuhusu mtu anayefanya uhalifu wa kutumia silaha, lengo likiwa ni kuhakikisha mkoa huo unabaki kuwa shwari.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa kanda hiyo Muliro Jumanne leo Juni 23, 2021 ambapo amesema kwamba siri ya mtoa taarifa itatunzwa na pesa hizo atapatiwa kwa siri bila kuzungushwa

Amesema kuwa mwananachi atakayetoa taarifa za kweli kwa jeshi la Polisi kuhusu watu wanaojihusisha na vitendo unyanganyi wa silaha na wakikamatwa basi Jeshi hilo litatoa pesa taslimi millioni 2 kwa mtoa taarifa.

“Tumeamua kutangaza donge nono la zawadi ambazo tutawapatia kwa siri watakaotuletea taarifa za kweli zilizosahihi za kuwakamata katika mazingira yoyote watu wanaojihusisha na vitendo vya unyang’anyi wa kutumia silaha, na wakikamatwa pamoja na silaha zao, tutatoa milioni 2 palepale mchezo ukikamilika anapewa pesa yake hakuna mzunguko na hili ni zoezi endelevu,” amesema Kamanda Muliro.

Aidha, Kamanda Muliro amewataka wahalifu Jijini Dar es Salaam kuchagua mambo mawili kuendelea kuingia kwenye msuguano na jeshi la polisi ama kuwa raia wema.

RC Makalla awahimiza watumishi kukopa, kuanzisha miradi
Mmiliki gari lilosababisha ajali na kuua 9 apewa saa 24 kujisalimisha